Muhtasari wa Gazeti la Taifa Leo Alhamisi Julai 10,2025
Ukurasa wa 1: Rais William Ruto ameonja viongozi wa upinzani kwamba hatakubali njama za kumwondoa madarakani kwa njia zisizo za kikatiba. Amesema amekuwa kimya lakini sasa amejiandaa kukabiliana nao kwa nguvu ili kuzuia ghasia.
Ukurasa wa 2: Kaunti 12 zimetengewa Sh 4.46 bilioni kwa miradi ya maendeleo katika mwaka wa kifedha 2025/2026.
Katibu wa Ardhi Nixon Korir na Mbunge Paul Chebor wamezuiwa kuvamia shamba la familia ya Rais wa zamani Daniel Arap Moi huko Nakuru.
Ukurasa wa 3: Mahakama kuu imezuia serikali kufunga Jiji la Nairobi wakati wa maandamano.
Watu sita waliohukumiwa kwa mauaji ya Mbunge George Thuo wakiachiwa kwa dhamana ya Sh milioni 1 wakisubiri rufaa.
Ukurasa wa 4: Gavana wa Makueni, Mutula Kilonzo, amesema KEMSA haina uwezo wa kusambaza dawa kwa kaunti kwa wakati.
Kaunti ya Homa Bay ikiwa na mradi wa kupanua barabara kuu za Rongo-Homa Bay na Homa Bay-Kendu Bay.
Ukurasa wa 5: Wauguzi zaidi ya 600 Kaunti ya Kilifi wameanza mgomo kutokana na malalamishi yao.
NEMA yapeleleza ombi la kujenga jaa la taka za asbestos eneo la Kalumani/Mnyenzeni katika Kaunti ya Kilifi.
Ukurasa wa 6-7: Makala ya tahariri inaonya juu ya mzozo kati ya Rais Ruto na Rigathi Gachagua kuwa hatari kwa nchi, ikisema Kenya iko katika mkondo wa mzozo usiopo kikomo.
Ukurasa wa 8: Kizza Besigye amezindua chama kipya cha kisiasa, People’s Front for Freedom (PFF), huku akiwa kizuizini Uganda.
Mafuriko Texas yakisababisha vifo vya watu 109 na wengine kukimbilia miti.
Ukurasa wa 9: Mrembo mmoja amekosana na mpenzi wake baada ya kumtaka “atungue mimba yake,” huku ukurasa wa 18 ukimtangazia mkulima Dennis Kipkoech kuwa mshindi wa jackpot ya Sh milioni 10.
Ukurasa wa 20: Chelsea ina nafasi nzuri ya kushinda kombe la klabu Bingwa Duniani, huku Rais Donald Trump akitarajia kuhudhuria fainali hiyo baada ya FIFA kufungua ofisi katika Trump Tower.