Muhtasari wa Gazeti la Taifa Leo Julai 9,2025
Ukurasa wa 1
Polisi walitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia waliokuwa wakiandamana katika maandamano ya Saba Saba.
Maandamano hayo yamewacha taifa katika huzuni kutokana na vifo vya raia wasiokuwa na hatia.
Ukurasa wa 2
Polisi washtusha kwa ukatili wakizima fujo.
Polisi walifyatua risasi kiholela, na kuua watu wasiohusika moja kwa moja na maandamano.
Mtoto wa miaka 12 aliuliwa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya nyumba yao huko Ndumberi, Kaunti ya Kiambu.
Ukurasa wa 2
OHCHR wametoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji ya zaidi ya watu 11 waliouawa Julai 7.
Ukurasa wa 2
Ripoti zinaeleza kuwa baadhi ya uporaji ulikuwa wa kupanga, huku baadhi ya wafanyabiashara wakilengwa kimakusudi.
Ukurasa wa 3
Raila akosolewa kutaka mageuzi mapya kwa polisi.
Wataalamu na viongozi wanasema tayari kuna ripoti zinazoweza kutumika kurekebisha huduma ya polisi badala ya kuanzisha mageuzi mapya.
Ukurasa wa 3
Jaji Mkuu Martha Koome amewataka raia na maafisa wa usalama kutekeleza majukumu yao kwa heshima ili kulinda amani na demokrasia.
Ukurasa wa 4
Wananchi waliandamana wakitaka Bw. Gitonga Mukunji aachiliwe baada ya kukamatwa kwa madai ya kuchochea ghasia.
Ukurasa wa 4
Bi Rachel Ruto amekiri kwamba ahadi nyingi za kisiasa hazilingani na hali halisi mashinani.
Ukurasa wa 6
Maadhimisho ya Saba Saba hayakuhitaji maandamano
Mhariri anahoji kuwa maadhimisho ya kihistoria hayakupaswa kugeuka ghasia.
Wanasiasa wasiteke maandamano ya vijana wanaotaka mabadiliko nchini
Vijana wa Gen Z wanaongoza vuguvugu la mabadiliko, hivyo si vyema kwa wanasiasa kuyatumia maandamano kwa manufaa yao binafsi.
Ukurasa wa 14
Ufugaji wa nyuki umechangia katika uhifadhi wa mazingira na kurejesha miti ya asili.
Ukurasa wa 15
Serikali yasambaza mbuzi kwa watu walioathiriwa na kiangazi Kajiado
Hatua hii inalenga kusaidia familia zilizoathiriwa na ukame kujiendeleza kiuchumi.